Sera ya Faragha Asus
ASUSTeK COMPUTER INC. na makampuni washirika (hapa itajulikana kama “ASUS”, “sisi/yetu”) tuna nia ya kuhakikisha tunalinda na kuheshimu faragha yako. Tunajitahidi kuendana na sheria zote husika za kulinda faragha na usalama wa data zako binafsi. Sera ya faragha ya ASUS, pamoja na notisi au matangazo yoyote ambayo yana taarifa za ziada zinazohusiana na bidhaa fulani za ASUS na huduma unayotumia (hapa itajulikana kama "Sera ya Faragha"), inabainisha hatua zetu za faragha kuhusu kukusanya, kutumia na kulinda data zako binafsi kupitia bidhaa na huduma za ASUS, tunazozitoa mtandaoni na nje ya mtandao. Katika Sera ya faragha, pia tunaeleza ni nani tunayeweza kumpa au kumwonyesha data binafsi iliyokusanywa.
Ikiwa wewe ni mtoto, unapaswa kufikia au kutumia bidhaa za ASUS na huduma baada ya wazazi wako (au mlezi wako) kusoma na kukubaliana na Sera yetu ya Faragha na kukubali kutoa data zako binafsi kwa ASUS.
1. Data zinazokusanywa na ASUS na jinsi ASUS inavyotumia data hizo
Kifungu hiki kinabainisha ni data zako zipi zinazoweza kukusanywa na ASUS na jinsi ASUS inavyoweza kutumia data hizo kwenye huduma na bidhaa za ASUS.
Unapotumia bidhaa za ASUS na huduma (kwa mfano, kompyuta za ASUS, programu, tovuti rasmi na huduma za usaidizi kwa wateja), tunaweza kuhitaji kukusanya data fulani binafsi kutoka kwako unapotumia au kuingiliana na bidhaa za ASUS na huduma.
Yafuatayo ni maelezo ya jumla ya data binafsi zinazoweza kukusanywa na ASUS na jinsi ASUS inavyoweza kutumia data hizo zilizokusanywa. Tafadhali fahamu kuwa tutakusanya baadhi tu ya vipengele vya data zako binafsi kwa madhumuni maalumu kulingana na bidhaa za ASUS na huduma ambazo utazitumia. Tafadhali fahamu kuwa vipengele vya taarifa binafsi zitakazokusanywa zitatofautiana kulingana na aina ya bidhaa na huduma. Zaidi ya hayo, katika nchi nyingine, ili kuepuka kukusanya na kutumia vibaya data za binafsi za watoto, huenda ukatakiwa kuweka umri wako au taarifa za mawasiliano ya wazazi wako (au mlezi) ili tuweze kupata idhini kutoka kwa wazazi wako (au mlezi ). Zaidi ya hayo, unapotumia bidhaa za ASUS na huduma, tunaweza kukusanya data fiche zifuatazo ambazo hazikutambulishi moja kwa moja au kwa usahihi.
Unapotumia bidhaa na huduma za ASUS, huhitajiki kutoa data zako binafsi kulingana na ombi lako. Hata hivyo, ikiwa utachagua kutokutoa data zako binafsi kwa ASUS, tunaweza kushindwa kutoa bidhaa na huduma husika za ASUS ili kukidhi mahitaji yako.
1.1 Data binafsi zinazokusanywa na ASUS
Data binafsi inamaanisha data yoyote ambayo inaweza kukutambulisha moja kwa moja au si moja kwa moja, kama jina lako, anwani ya barua pepe na anwani ya IP. ASUS inaweza kukusanya data zako binafsi zifuatazo kulingana na ridhaa yako ya awali:
- Data zako za kweli, sahihi, za sasa na kamili za usajili, ikiwa ni pamoja na anwani yako ya barua pepe, nchi / eneo na umri (sasa imeombwa tu katika baadhi ya nchi) unapojiunga na akaunti ya Mwanachama ya ASUS. Ikiwa unatumia akaunti yako ya mitandao ya kijamii (kwa mfano, akaunti yako ya Facebook au Google) kujiandikisha kwa ajili ya akaunti ya Wanachama wa ASUS, mtoa huduma wa huduma hiyo ya mtandao wa kijamii (kwa mfano, Facebook Inc. au Google Inc.) anaweza kutoa data zako binafsi zilizoko kwenye akaunti ya mitandao kijamii (kwa mfano, anwani ya barua pepe, jina, jina la utani na tarehe ya kuzaliwa) kulingana na idhini yako. Aidha, unapoingia kwenye akaunti yako ya Mwanachama wa ASUS (Njia: Tembelea tovuti rasmi ya ASUS http://www.asus.com → tafuta "INGIA" upande wa juu wa kulia wa wavuti → ingiza anwani ya barua pepe na nenosiri ulilolisajili kwenye akaunti ya ASUS ya mwanachama ili ufikie ata zako chini ya “Akaunti ya ASUS”), unaweza kutoa data zako za ziada za binafsi ili kuhariri wasifu wako wa akaunti ya Mwanachama wa ASUS (kwa mfano, picha yako, jinsia, anwani na taaluma), na kufurahia bidhaa na huduma za ASUS zilizounganishwa na akaunti yako ya Mwanachama wa ASUS (kwa mfano, namba yako ya utambulisho ya bidhaa kwa ajili ya usajili wa bidhaa za ASUS, makala na picha zilizochapishwa na kupakiwa kwenye majukwaa ya mijadala ya ASUS ambavyo vinaweza kuwa na data zako binafsi).
- Jina lako, anwani ya barua / usafirishaji / anwani ya bili (ikiwa ni pamoja na msimbo wa zip), data za mawasiliano, anwani ya barua pepe, namba ya kadi ya kifedha au data nyingine za huduma ya malipo wakati wa manunuzi ya bidhaa zetu (kwa mfano, ununuzi wa bidhaa za ASUS kupitia Duka la ASUS) na huduma za kulipiwa. Zaidi ya hayo, pamoja na data binafsi, data yako ya bidhaa (kwa mfano, namba ya bidhaa, namba ya IMEI) zinaweza pia kukusanywa unapoomba huduma fulani za wateja (kwa mfano, huduma za ukarabati wa bidhaa).
- Jina lako, taarifa za mawasiliano, barua pepe, jinsia, tarehe ya kuzaliwa,taarifa za bidhaa (kwa mfano, nambari ya utambulisho ya bidhaa, Nambari ya IMEI), na nakala ya ankara yako (katika baadhi ya nchi, jina lako, anwani na data nyingine za binafsi zinaweza kuingizwa katika ankara yako), unapoingia kwenye matukio yetu au kampeni. Vitu husika vya data yako binafsi vitakavyokusanywa vitatofautiana kutokana na tukio au kampeni husika. Zaidi ya hayo, kama wewe ni mshindi wa tukio au kampeni yetu, au kama utapokea zawadi kutoka kwa ASUS, huenda ukahitajika kuongeza anwani yako ya barua / usafirishaji (ikiwa ni pamoja na msimbo wa zip) na data binafsi kwa tamko la kodi (kwa mfano, anwani yako ya makazi, ID au namba ya pasi ya kusafiria na nakala yake).
Zaidi ya hayo, pamoja na data binafsi, unaweza kuhitajika kutoa taarifa za akaunti yako ya benki wakati unapojiunga na tukio letu linalohusu kupokea pesa. - Umri wako, jinsia, urefu, uzito, joto la mwili, mapigo ya moyo, shinikizo la damu mjongeo wa tumbo pamoja na data fulani kuhusu shughuli zako za kila siku, kwa mfano, hatua uliyopiga, kalori ulizotumia, ratiba yako ya kulala na taarifa zako za kila siku wakati unapotumia vifaa na huduma zetu za kiafya.
- Data yako ya bidhaa, kama vile nambari ya utambulisho ya bidhaa, Anwani ya IP, Anwani ya MAC, Nambari ya IMEI, Nambari ya ID ya Android na vitambulisho vingine vya kipekee vinaweza kukusanywa wakati unatumia bidhaa za ASUS.
- Data yako ya eneo inayohusishwa na bidhaa za ASUS na huduma, kama vile mawasiliano yako ya GPS, data zinazobainisha vyanzo vya karibu vya Wi-Fi na minara ya simu, nchi, mji, ukanda saa, latitudo, longitudo, mwinuko toka usawa wa bahari na usawa bidhaa ilipo, kasi ya mjongeo wa bidhaa yako, mipangilio ya nchi yako na lugha kwenye bidhaa yako.
- Sauti yako, video, kumbukumbu za mawasiliano wakati unawasiliana na ASUS (kwa mfano, kwa kupiga simu kituo cha simu cha ASUS, kwa kutumia kituo cha mtandaoni cha huduma kwa wateja cha ASUS kuwasiliana na ASUS, kujaza fomu ya maombi mtandaoni kwenye tovuti rasmi ya ASUS na kutuma barua pepe kwa ASUS) . Aidha, tunaweza kurekodi picha yako kupitia kamera za usalama wakati unapotembelea vituo vya matengenezo vya ASUS Royal Club na ofisi za ASUS. Zaidi ya hayo, tunaweza kukusanya maelekezo ya sauti yako na rekodi ya video yako ambayo inaweza kuwa na picha ya mazingira yako ya nyumbani unapotumia bidhaa na huduma zetu zinazohusiana na roboti. Sauti hii, video na kumbukumbu za mawasiliano yako zinaweza kuwa na taarifa zako binafsi.
1.2 Jinsi ASUS inavyotumia data zako binafsi
Tunaweza kutumia data zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:
- Kutathmini na kuboresha bidhaa na huduma za ASUS.
- Kupata maoni ya wateja na kuchambua uzoefu wa mtumiaji kwa lengo la kuendeleza na kutathmini bidhaa na huduma mpya.
- Ili kutimiza mchakato wa usajili wa akaunti ya Mwanachama wa ASUS na kupata bidhaa za ASUS na huduma zinazohusiana na akaunti ya mwanachama wa ASUS (kwa mfano, usajili wa bidhaa na huduma za majukwaa ya majadiliano ya ASUS).
- Kutoa huduma za uwasilishaji (kwa mfano, uwasilishaji wa ankara ya udhibitisho wa manunuzi), sasisho za programu na matangazo ya kiufundi kwa ajili ya bidhaa za ASUS na huduma utakazonunua.
- Ili kushughulikia na kukamilisha usajili wowote uliojiunga nao, ikiwa ni pamoja na eDMs za ASUS au majarida ili kukuwezesha kupata habari za hivi karibuni za ASUS, matangazo na matukio yajayo. Unaweza kujiondoa wakati wowote bila gharama.
- Ili kukutumia taarifa muhimu, kama vile mawasiliano juu ya mabadiliko ya vigezo vyetu, masharti na sera. Kwa sababu ya umuhimu wa mawasiliano haya, huwezi kujiondoa kwenye kupokea mawasiliano haya.
- Ili kuthibitisha utambulisho wako, kutoa viingilio vya matukio au kampeni na tuzo, kuwasiliana nawe kuhusu maswala yanayohusu kampeni au tukio, kufanya malipo, kubainisha kodi na kutoa huduma za usafiri na kukukinga kwa bima ikiwa ni lazima wakati unapoingia kwenye matukio yetu au mashindano.
- Ili kukusaidia kurekodi, kuchambua, kurekebisha na kuhifadhi taarifa ikiwa ni pamoja na data za mwili wako, shughuli zako za kila siku na matokeo ya shughuli hizo kutokana na mahesabu ya data hapo juu. Zaidi ya hayo, tutakusaidia kwenye uhariri na kupata data na matokeo ya shughuli, wakati unaposhirikisha data hizi kwa familia yako, waangalizi, na wataalamu wa huduma za afya.
- Kukupa huduma za usaidizi kwa wateja (kwa mfano, kutimiza maombi yako ya matengenezo na kujibu maswali yako), huduma yetu kwa wateja na uchambuzi wa utafiti wa kuridhika kwa wateja, na kulinda haki zako na matakwa yako na kupokea utawala wa ufikiaji, tunaweza kuchukua sauti yako, mawasiliano ya recodi za video unapowasiliana na ASUS au unapotembelea vituo vy ya matengenezo vya ASUS au ofisi za ASUS. Zaidi ya hayo, tunaweza kukusanya sauti yako na rekodi za video yako ili kusaidia bidhaa na huduma zinazohusiana na roboti kufika kwenye eneo fulani kulingana na hitaji lako.
- Ili kukupa huduma za masoko zilizobinafsishwa, kwa mfano, kutumia vidakuzi vya matangazo vya watu wengine ili kutoa mawasiliano ya masoko na matangazo ambayo tunaamini yanaweza kuwa na manufaa kwako, au mapendekezo kuhusu huduma ambazo zinaweza kukuvutia kulingana na matumizi yako ya bidhaa na huduma za ASUS .
- Madhumuni mengine yoyote kwa idhini yako ya awali.
1.3 Data fiche inayokusanywa na ASUS na jinsi ASUS inavyotumia data fiche hiyo
Data fiche inamaanisha data yoyote ambayo haiwezi kukutambulisha moja kwa moja au kwa usahihi, kama vile modeli ya bidhaa yako, toleo la programu na tarehe ya ankara. Unapotumia bidhaa za ASUS na huduma, tunaweza kukusanya data fiche zifuatazo kutoka kwako, na kutumia data fiche hiyo kwa madhumuni yoyote. Zaidi ya hayo, wakati data fiche zifuatazo zinapokusanywa pamoja na data zako binafsi zilizoorodheshwa hapo juu, katika mazingira hayo, tutazichukulia data fiche hizo kama data binafsi na kulinda data fiche hizo kwa kiwango cha ulinzi wa data binafsi.
- Data zako za logi zinazohusishwa na bidhaa za ASUS na huduma, kama vile jina la modeli yako ya bidhaa, jina la bidhaa, jina la chapa, jina la mtengenezaji, namba ya kifaa, aina na toleo la vifaa (kwa mfano, CPU na motherboard) na mfumo endeshi, mipangilio ya msingi ya kiwandani, wakati wa uwezeshwajii, data za usasishwaji wa programu ya msingi ya kudumu (kwa mfano, njia ya utekelezaji wa usasishaji wa programu ya msingi ya kudumu, tarehe ya usasishaji na matokeo ya usasishaji), ukubwa wa kihifadhi kumbukumbu, data zinazohusiana na Kihifadhi kumbukumbu cha kudumu (ROM) (kwa mfano, aina, toleo, uundwaji na maelezo ya ROM), uwezo wa kamera, rangi ya bidhaa, mawasiliano ya simu na mtandao unayotumia kuunganisha bidhaa na huduma zetu, hali ya mtandao, data za logi ya simu, hali ya kusimama, kumbukumbu ya hitilafu, kiolesura kilichopendelewa, aina, toleo na mipangilio ya lugha ya kivinjari, uchunguzi na matumizi ya data, tabia yako ya matumizi, toleo la GPS na Wi-Fi, hali ya mfumo (kwa mfano, hali ya matumizi ya betri, CPU na RAM), na muda wa eneo husika.
- Data za programu zako zinazohusishwa na matumizi yako na muingiliano na programu za ASUS, kama vile jina na toleo la programu, muda wa kusakinisha na kusakinua, muda wa kuingia na kutoka, marudio na idadi ya matumizi yako, wakati wa kufungua na kufunga programu, kategoria ya programu zako unazopendelea, mipangilio ya tabia ya matumizi, toleo la sasisho na matokeo ya sasisho.
- Data zako za ununuzi wa bidhaa na huduma za ASUS (kwa mfano, tarehe ya ununuzi na jina la muuzaji) unapoomba huduma fulani za msaada kwa wateja (kwa mfano, huduma za ukarabati wa bidhaa) au kujiunga na matukio yetu.
2. Utunzaji wa data zako binafsi
Kifungu hiki kinaelezea ni kwa muda gani ASUS itatunza data zako binafsi.
Tutatunza data zako binafsi kwa wakati muhimu unaohitajika ili kutimiza malengo yaliyotajwa katika Sera hii ya faragha, vinginevyo muda mrefu zaidi wa kuhifadhi utaruhusiwa kisheria au utahitajika kutimiza malengo mengine muhimu. Kwa mfano, kwa lengo la usimamizi wa uhusiano wa wateja, tunaweza kuhifadhi data zako binafsi ndani ya muda wa kutosha na wa kuridhisha; ili kuzingatia sheria ya kodi au sheria na kanuni zingine, tunaweza kuhifadhi data zako binafsi ndani ya kipindi kilichoombwa na sheria na kanuni hizo; kutokana na maombi kutoka kwa serikali au mahakama kwa madhumuni kama vile uchunguzi au kesi, tunaweza kuhifadhi data zako binafsi kwa muda mrefu zaidi. Zaidi ya hayo, ikiwa unataka kuondoa idhini yako ya awali ya kukusanya data zako binafsi kwa ASUS, tutaacha kukusanya data zako binafsi kwa ombi lako na tutahifadhi tu data zako binafsi zilizokusanywa kabla ya ombi hilo la kujiondoa.
3. Ni nani anayeonyeshwa data zako binafsi na ASUS
Kifungu hiki kinaeleza kuwa ASUS inaweza kushirikisha watu wengine data zako katika mazingira na makusudi yenye ukomo.
Data zako binafsi hazitaonyeshwa kwa watu wengine wowote bila haya yafuatayo:
3.1 Idhini Yako
- Tutaonyesha au kushirikisha tu data zako kwa wengine kwa idhini yako ya awali.
3.2 Washirika wa Kibiashara
- Tunaweza kuonyesha data zilizofichwa utambulisho kwa washirika wetu wa kibiashara, kwa mfano, washirika wa kibiashara ambao hutoa huduma za uchambuzi wa data au matangazo na mawasiliano ya masoko kwa kutegemea data zilizofichwa au kuondolewa utambulisho kupitia vidakuzi vya matangazo vya watu wengine.
3.3 Watoa Huduma
- Tunaweza kuonyesha na kushirikisha vitu muhimu vya data zako binafsi kwa watoa huduma wetu ambao hutoa huduma au kwa niaba yetu, kwa mfano, mashirika ya masoko yanayotusaidia na kutuma mawasiliano ya masoko na kufanya matukio/kampeni za masoko, makampuni ya usambazaji yanayowasilisha bidhaa ulizonunua, watoa huduma za malipo wanaochakata malipo yako, na watoa huduma kwa wateja wanaotoa huduma kwa wateja kwako (kwa mfano, huduma za kutengeneza bidhaa, huduma kupitia kituo cha simu cha ASUS na mfumo wa mtandaoni wa huduma kwa wateja wa ASUS). Watoa huduma hawa watatumia data zako binafsi tu kwa kufuata maelekezo yetu na kwa upeo wa madhumuni haya; ASUS inahakikisha kwamba watoa huduma zetu wote wanazingatia Sera ya Faragha.
3.4 Kwa madhumuni ya kisheria, ulinzi, na kiusalama
Tunaweza kuonyesha au kushirikisha baadhi ya data zako muhimu kwa watu wengine kutokana na moja kati ya madhumuni ya kisheria au kiusalama yafuatayo:
- Kwa kiwango kinachohitajiwa na sheria husika au kanuni au mamlaka ya serikali au mamlaka ya mahakama, kinachotosha kuanzisha au kuhifadhi madai ya kisheria au ulinzi, au kinachotosha kuzuia udanganyifu au shughuli nyingine haramu.
- Ili kulinda haki, mali au usalama wa ASUS, watoa huduma wetu, wateja au umma, kama inavyohitajiwa au kuruhusiwa kisheria.
4. Ushughulikiaji unaovuka mipaka wa data zako binafsi
Aya hii inaeleza jinsi ASUS inavyoweza kuhamisha data zako binafsi kutoka nchi tofauti chini ya ofisi ambazo ASUS inapaswa kuzingatia sheria za faragha na kanuni katika nchi hizo.
Unaelewa na unakubaliana kuwa unapotoa data zako binafsi kwa ASUS, data zako binafsi zinaweza kuhamishwa, kuhifadhiwa, kutumiwa au kuchakatwa na ASUS na kampuni yoyote inayohusiana nayo, watoa huduma ambao wanaweza kuwa katika nchi tofauti na wewe. Uhamisho wote ulioelezwa, uhifadhi, au mchakato wa data zako binafsi, utakuwa chini ya Sera ya Faragha na sheria zinazohusika juu ya ulinzi wa faragha na usalama wa data binafsi.
5. Vidakuzi (Cookies) na teknolojia zinazofanana nayo
Kifungu hiki kinaelezea jinsi ASUS na watu wengine hutumia vidakuzi na teknolojia zinazofanana na hii kwenye bidhaa na huduma za ASUS, na jinsi unavyoweza kusimamia mipangilio ya vidakuzi.
ASUS na washirika wetu hutumia vidakuzi (vidakuzi ni mafaili madogo ya maandishi yaliyowekwa kwenye bidhaa zako ili kubinafsisha matumizi yako kwenye bidhaa na huduma za ASUS) na teknolojia zinazofanana hiyo kama vile beacons za mtandao ili kutoa bidhaa na huduma zetu kwako. Unapotembelea moja kati ya tovuti zetu chini ya anwani ya wavuti ya ASUS (ikiwa ni pamoja na tovuti ndogo na matoleo ya nchi / eneo fulani), tovuti hiyo ya ASUS inaweza kutumia baadhi au vidakuzi vifuatavyo au teknolojia zinazofanana navyo.
Takriban data zote zilizokusanywa kupitia vidakuzi zitahifadhiwa tu katika bidhaa zako, badala ya kutumwa kwa ASUS. Katika mazingira adimu sana pekee, data zilizokusanywa kupitia vidakuzi zinaweza kutumwa kwa ASUS. Kwa mfano, unaponunua bidhaa zetu kwenye Maduka ya ASUS, tunaweza kutumia vidakuzi kukusanya anwani zako za IP wakati wote unapoingia na kuweka ombi la ununuzi kwenye Duka la ASUS, ili kuthibitisha mtumiaji anayeweka ombi hiyo ni sawa na aliyeingia kwenye Duka la ASUS kwa ajili ya usalama wa ununuzi mtandaoni.
5.1 Jinsi tunavyotumia Vidakuzi
1. Ili kuimarisha na kukamilisha uzoefu wako mtandaoni, tunatumia vidakuzi vifuatavyo ambavyo ni muhimu kwa ajili ya bidhaa na huduma za ASUS:
Kazi | Mfano |
Kujisajili na kuthibitisha | Tunatumia vidakuzi kuhifadhi namba yako ya kipekee ya ID na data za uthibitishaji kwenye bidhaa zako. Vidakuzi vinakuwezesha kutembelea na kuhama kutoka ukurasa mmoja hadi mwingine ndani ya bidhaa na huduma za ASUS bila kuingia tena ili kuona kurasa zifuatazo, kama vile vidakuzi vya tiketi vitolewavyo na ASUS. |
Huhifadhi mapendekezo yako na mipangilio | Tunatumia vidakuzi ili kudumisha mipangilio na mapendekezo yako kwenye bidhaa zako, kama lugha yako unayoipendelea, eneo au mwandiko; kwa kuhifadhi mipangilio katika vidakuzi, sio lazima kuomba mapendeleo na mipangilio yako kila wakati unapotembelea bidhaa na huduma zetu, kama vile vidakuzi vya current_site na vidakuzi vya EntryPage vinavyotolewa na ASUS. |
Matumizi ya ingizo la mtumiaji | Tunatumia vidakuzi kuhifadhi kwa muda data unazoingiza kwenye bidhaa na huduma za ASUS, kama vile vidakuzi vihesabuji vinavyotolewa na ASUS. Kwa mfano, unapofurahia mchakato wa maununuzi yako kupitia Duka la ASUS, vidakuzi vitakusaidia kukumbuka bidhaa na kiasi ulichokibofya na data unayoingiza. |
Usalama | Tunatumia vidakuzi ili kulinda usalama wa shughuli zako za ununuzi mtandaoni, kama vile vidakuzi vya ip_address vinavyotolewa na ASUS. Kwa madhumuni hayo hapo juu, unaponunua bidhaa zetu kupitia Duka la ASUS, tunaweza kuhifadhi anwani zako za IP ndani ya ASUS ili kutusaidia kuthibitisha mtumiaji ambaye ameweka ombi la manunuzi kwenye Duka la ASUS kama ni sawa na yule anayeingia kwenye Duka la ASUS. |
Kuweka msawazisho wa mzigo | Tunatumia vidakuzi kwa ajili ya kuweka msawazo wa mzigo ili kukupa utumizi unaofaa wa kuvinjari kwenye tovuti zetu, kama vile kidakuzi cha BigipServerNew kinachotolewa na ASUS. |
2. Kwa madhumuni ya uchanganuzi na kukupa huduma za matangazo zilizobinafsishwa pamoja na kazi nyingine, tunatumia vidakuzi vifuatavyo ili kuboresha utumizi wako wa kutumia bidhaa na huduma za ASUS:
Kazi | Mfano |
Uchanganuzi | Tunatumia vidakuzi ili kuhesabu idadi na urefu wa utembeleaji wako katika bidhaa na huduma za ASUS pamoja na ni sehemu gani au ni vipengele gani ulivyovitembelea pia. Data hii inatusaidia kuchambua utendaji na uendeshaji wa bidhaa na huduma za ASUS ili kuboresha utendaji na kuendeleza vipengele vipya, kazi na huduma, kama vile vidakuzi vya MIGO vinavyotolewa na MIGO Corp., vidakuzi vya Google Tag Manager na vidakuzi vya Google Analytics vinavyotolewa na Google Inc. Kwa madhumuni hayo hapo juu, unapoperuzi tovuti zetu, tunaweza kuhifadhi data zako binafsi kama anwani ya IP na Kitambulisho cha Mwanachama wa ASUS ndani ya ASUS kwa njia ya vidakuzi tajwa hapo juu vya MIGO. |
Kulenga na kutangaza | Tunatumia vidakuzi kukusanya data kuhusu matumizi yako ya bidhaa na huduma za ASUS na kutambua maslahi yako, kama vile matangazo uliyotazama. Vidakuzi hivyo pia hutumiwa kutawala idadi ya mara unazoona tangazo pamoja na kusaidia kupima ufanisi wa kampeni za matangazo. ASUS huweka vidakuzi kwa kutumia huduma za kampeni ya matangazo, kama Hubrus DSP inayotolewa na Hubrus, vidakuzi vya Google AdWords na vidakuzi vya Google Double Click vinavyotolewa na Google Inc. Data zinazokusanywa na vidakuzi hutumiwa tu kati ya ASUS na watoa huduma za kampeni za matangazo. |
Kuangalia video za YouTube zilizowekwa kwenye tovuti zetu | Tunatumia vidakuzi kutusaidia kuweka video za YouTube kwenye tovuti zetu. Unaweza kutazama video za YouTube kupitia tovuti zetu zenye vidakuzi vile vinavyotolewa na Google Inc. |
5.2 Jinsi ya kutawala mipangilio ya vidakuzi
- Tafadhali kumbuka kwamba unaweza kusanidi mipangilio ya vidakuzi kwa kufikia kivinjari ulichosakinisha ili kukubali, kuzuia au kufuta baadhi au vidakuzi vyote (kwa mfano, vidakuzi vya watu wengine).
- Katika baadhi ya nchi, kwa mara ya kwanza unapoperuzi tovuti za ASUS, tunaweza kuweka utangulizi mfupi juu ya jinsi tunavyotumia vidakuzi kwenye ujumbe uliowekwa kwenye upande wa juu wa tovuti hizo za ASUS. Unaweza kuchagua kwa hiari kukubali au kuzuia vidakuzi vya watu wengine kupitia ujumbe huo.
- Ikiwa ungependa kuzuia vidakuzi, unaweza kushindwa kutumia vipengele vyote vya bidhaa na huduma za ASUS.
- Kazi za mipangilio ya vidakuzi zinaweza kutofautiana kulingana na aina na toleo la kivinjari ulichosakinisha. Tumejaribu kuorodhesha aina zifuatazo za vivinjari maarufu na zilizozoeleka. Unaweza kurejea kiunganishi hiki kuelewa jinsi ya kutawala mpangilio wa vidakuzi kwenye kivinjari chako (Maudhui ya kiunganishi hiki yako katika lugha ya Kiingereza) Kurahisisha usomaji wako, tafadhali tafuta chaguo la lugha katika ushirikifu ufuatao ili kuchagua lugha yako unayoipendelea). Pia, ikiwa hutumii moja kati ya vivinjari vifuatavyo, au yaliyomo katika viunganishi vifuatavyo yameondolewa au hayapatikani, tafadhali tembelea kurasa za matamko ya faragha ya vivinjari hivyo au kurasa za usaidizi kwa maelezo zaidi. Unaweza pia kurejelea https://www.aboutcookies.org/ (yaliyomo katika kiunganishi hiki yako katika lugha ya Kiingereza) ambayo inaeleza jinsi ya kutawala mipangilio yako ya vidakuzi kupitia vivinjari mbalimbali.
5.3 Beacon za Mtandao
Web beacon ni picha angavu ya GIF au PNG yenye ukubwa wa pikseli 1x1 inayowekwa kwenye tovuti au barua pepe ili kupima ufanisi wa kampeni fulani. ASUS au watoa huduma wetu wanaweza kutumia web beacons kujua kama unatembelea baadhi ya kurasa au kubonyeza viungo kwenye bidhaa na huduma za ASUS. Tunaweza kuweka web beacons kwenye mawasiliano yetu ya masoko kama vile eDMs au majarida ya ASUS ili kujua ni yapi kati ya yaliomo ambayo umeyafungua au kuyasoma. Tutatumia data kutoka kwa beacons za mtandao ili kuboresha tovuti zetu, bidhaa na huduma za ASUS.
6. Viunganishi vya watu wengine kwenye bidhaa na huduma za ASUS
Kifungu hiki kinaeleza kuwa wakati unapotembelea kiunganishi au kutumia huduma zingine zinazotolewa na watu wengine, tafadhali daima urejelee sera zinazohusiana na faragha zilizotolewa na watu wengine.
Bidhaa na huduma za ASUS zinaweza kuwa na viunganishi vya tovuti za watu wengine. Tafadhali fahamu kuwa ASUS haitawajibika kuhusu usalama, vitendo vya faragha na vifaa vya tovuti hizo za watu wengine. Tunakuhimiza uchukue tahadhari wakati unatoka kwenye tovuti yetu, na kusoma sera za faragha za tovuti hizo nyingine kwa makini. Sera hii ya Faragha inatumika kwenye bidhaa na huduma za ASUS tu.
7. Usalama
Kifungu hiki kinaeleza jinsi ASUS inavyolinda data zako binafsi na kutoa baadhi ya mapendekezo juu ya jinsi ya kulinda data zako binafsi kwa upande wako.
Tunachukua tahadhari kulinda data zako binafsi dhidi ya kufikiwa kusikoidhinishwa, kubadilishwa, kuonwa au kuharibiwa. Tunafanya mapitio ya ndani ya ukusanyaji wetu wa data, kuhifadhi na hatua za uchakataji na mikakati ya kiusalama ya kiufundi na kimpangilio, pamoja na mikakati ya kiusalama ya miundombinu ili kujilinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa wa mifumo ambayo tunahifadhi data zako binafsi. Uhamishaji wa data kati ya maeneo tofauti ya ASUS na washirika wake wanaohusiana nao hufanywa kupitia mtandao wetu wa eneo pana uliolindwa. Unapowasilisha data yako binafsi, data yako binafsi inalindwa mtandaoni na nje ya mtandao. Hata hivyo, ASUS haiwezi kukuhakikishia ulinzi mkamilifu kwenye intaneti. Kulinda data zako binafsi kutokana na kufikiwa kusikoidhinishwa, tunapendekeza ufanye yafuatayo:
7.1 Ili kulinda kwa usahihi akaunti yako ya mwanachama wa ASUS, kwa mfano:
- Kutumia nywila zenye mchanganyiko wa herufi na namba wakati wa kujisajili kwa ajili ya akaunti ya Mwanachama ya ASUS.
- Kutumia jina lako la akaunti na nywila ili uingie kwenye akaunti ya Mwanachama ya ASUS. Pia wewe pekee unawajibika kikamilifu kwa kulinda usiri wa jina lako la akaunti na nywila na shughuli yoyote inayofanyika kwenye akaunti yako ya Mwanachama wa ASUS.
- Kubadilisha nywila zako za akaunti ya Mwanachama ya ASUS mara kwa mara.
- Kuwasiliana na sisi mara moja unapoona kwamba jina la akaunti / nywila ya akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS limetumika vibaya. ASUS inaweza kusimamisha au kufuta ruhusa ya kuingia kwenye akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS yenye jina la akaunti husika/nywila (au sehemu yake yoyote), na kuondoa data yako binafsi inayohusiana na akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS.
Kuhakikisha bidhaa zako zina masasisho ya karibuni (up to date) ili kukabiliana na dosari za kiusalama kwenye programu zako na kutumia programu kama zile za kujikinga na virusi.
7.3 Kama utabaini hitilafu ya kiufundi inayokabili bidhaa na huduma za ASUS, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia privacy@asus.com
8. Jinsi ya kusimamia data zako binafsi
Kifungu hiki kinafafanua kuwa ikiwa una maswali yoyote au maombi juu ya data zako binafsi zilizokusanywa na ASUS, unaweza kuingia kwenye “Akaunti yako ya ASUS” au kutawala mipangilio inayohusiana na faragha kwenye bidhaa husika za ASUS na huduma unayotumia. Pia, unaweza kuwasiliana nasi kupitia "Ombi la wateja juu ya data binafsi" kwenye tovuti rasmi ya ASUS au kwa kutuma barua pepe kwa privacy@asus.com.
8.1 Akaunti ya Mwanachama ya ASUS
- Tafadhali toa data zako za kweli, sahihi, za karibuni na kamili kwa ASUS kwenye akaunti yako ya Mwanachama wa ASUS ili ASUS iweze kukupa bidhaa na huduma stahiki za ASUS.
- Unaweza kuona na kubadilisha data za akaunti yako kwa kuingia kwenye akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS na kuhariri data za akaunti yako.
- Ikiwa ungependa kujiunga au kujiondoa kwenye eDM za ASUS na matangazo ya ASUS, bidhaa za hivi karibuni na huduma, unaweza kubadilisha mpangilio kwa kuingia kwenye akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS utafute "Jiunge" kwenye safu ya kushoto chagua "NDIO" au "HAPANA ". Ikiwa utachagua "HAPANA" kwa ajili ya kujiondoa, tafadhali fahamu kuwa inaweza kuchukua takriban siku 2 za kazi ili kukamilisha mchakato wa kujiondoa.
8.2 Bidhaa na huduma za ASUS
Uko huru kuchagua kuwezesha au kuzuia kutoa data zako binafsi kwa ASUS kupitia mipangilio ya faragha-kwenye bidhaa na huduma za ASUS wakati wowote unapotumia bidhaa na huduma hizo za ASUS.
8.3 Mipangilio ya vidakuzi (Tafadhali rejea “Jinsi ya kusimamia mipangilio ya vidakuzi” “Vidakuzi na teknolojia zinazofanana na hizo” katika Sera hii ya Faragha.)
- Unaweza kusimamia mipangilio ya vidakuzi kupitia kivinjari ulichosakinisha ili kukubali, kuzuia au kufuta baadhi au vidakuzi vyote (kwa mfano,vidakuzi vya watu wengine) au kupokea mipangilio mingine wakati wote.
- Ikiwa hutaki ASUS kukupa huduma za masoko na matangazo zilizobinafsishwa kwa njia ya vidakuzi vya watu wengine, unaweza kuzuia au kufuta vidakuzi vya watu wengine kupitia kivinjari chako wakati wote.
8.4 Wasiliana na ASUS ili kusimamia data zako binafsi
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia "Ombi la mteja juu ya data binafsi" kwenye tovuti rasmi ya ASUS au kupitia barua pepe kwa privacy@asus.com ikiwa una maombi na maswali yoyote kuhusu data zako binafsi chini ya akaunti yako ya Mwanachama ya ASUS au data nyingine za binafsi zilizokusanywa na ASUS, kama vile ombi la ufikiaji, kusahihisha, kupakua, kuzuia, kufuta, kukataa ASUS kutumia baadhi au data zako zote za binafsi ( kwa mfano, unaweza kuwasiliana na sisi ikiwa unafikiri ASUS inaweza kukusanya na kutumia data zako binafsi vibaya) na kuzuia ASUS kutumia data zako binafsi chini ya hali fulani (kwa mfano, unaweza kuwasiliana na sisi ikiwa hutaki data zako binafsi kuchambuliwa) wakati wote.
Pia, ikiwa umekubali ASUS kukusanya data yako binafsi kupitia bidhaa za ASUS na huduma, uko huru kuondoa ridhaa yako kwa kubadilisha mipangilio inayohusiana na faragha kwenye bidhaa na huduma husika za ASUS (tafadhali rejea 8.2 katika Sera hii ya Faragha) au kwa kuwasilisha ombi lako la uondoaji wa idhini kwetu. Tutaacha kukusanya data zako binafsi na kubaki tu na data zako binafsi zilizokusanywa kabla ya ombi hilo la kujiondoa.
8.5 Kila wakati unapotumia bidhaa na huduma za ASUS, tunajitahidi kudumisha usahihi wa data zako binafsi na kulinda data zako binafsi dhidi ya uharibifu wowote mbaya au wa bahati mbaya. Tutatunza maombi yako kuhusu data zako binafsi; hata hivyo, tunaweza kushindwa kukamilisha maombi yako hapo juu katika moja ya mazingira yafuatayo:
- Kama inavyotakiwa au kuruhusiwa chini ya sheria za maombi;
- Kwa malengo halali ya kibiashara;
- Maombi yasiyotabirika yanayojirudia ambayo yanahitaji jitihada za kiufundi na rasilimali nyingi, kwa mfano, kutengeneza mfumo mpya au kubadili utendaji kazi wa sasa wa msingi;
- Kunakoweza kuathiri faragha ya wengine;
Faragha ya Watoto
Kifungu hiki kinaeleza kuwa ili kulinda faragha ya watoto, ikiwa wewe ni mtoto, tafadhali tafuta idhini ya wazazi wako (au mlezi) kabla ya kutoa data zako binafsi kwa ASUS. Pia, ikiwa wazazi wako (au mlezi) wangependa kusimamia data zako binafsi, wanaweza kuwasiliana nasi kupitia "Ombi la wateja juu ya data ya binafsi" kwenye tovuti rasmi ya ASUS au kupitia barua pepe ya privacy@asus.com
Kwa kutambua hatukusanyi data binafsi kutoka kwa mtoto chini ya umri wa miaka kumi na sita (16), au umri wa kiwango cha chini katika mamlaka husika, bila idhini ya wazazi. Tunawahimiza wazazi (au mlezi) kuchukua jukumu kubwa juu ya shughuli na maslahi ya mtoto mtandaoni wakati wa kutumia bidhaa na huduma za ASUS.
Ikiwa wewe ni mtoto, tafadhali tafuta idhini ya wazazi kabla ya kutumia bidhaa na huduma za ASUS. Unaweza kuwasilisha data zako binafsi kwetu tu kwa idhini ya wazazi (au mlezi). Wazazi wako (au mlezi) wanaweza kuwasiliana nasi kupitia "Ombi la wateja juu ya data binafsi" kwenye tovuti rasmi ya ASUS au kupitia barua pepe kwa privacy@asus.com ili kurejesha au kuondoa idhini yoyote iliyotolewa awali, ombi la kufikia, kurekebisha, kupakua, kuzuia, kufuta, kukataa ASUS kutumia baadhi au data yako yoyote ya binafsi (kwa mfano, wazazi wako (au mlezi) wanaweza kuwasiliana nasi ikiwa wanaona ASUS inaweza kukusanya na kutumia data zako binafsi vibaya) na kuzuia ASUS kutumia data zako binafsi chini ya hali fulani (kwa mfano, wazazi wako (au mlezi) wanaweza kuwasiliana na sisi ikiwa hawataki data zako binafsi zichambuliwe) wakati wote.
10. Data Binafsi za Siri
ASUS kamwe haitakuomba kutoa data binafsi za siri (nyeti) kama vile data kuhusu rekodi yako ya matibabu au afya, msimamo wa kisiasa, imani za kidini au falsafa, makosa ya jinai (ya kutuhumiwa, au kufanya), uhalifu uliofanywa, asili au kabila, uanachama wa ushirika wa kibiashara, mwelekeo wa kijinsia, historia ya maswala ya kingono, tabia au data za maumbile. Tafadhali jiepushe dhidi ya kutupa data binafsi nyeti kama hizo.
11. Mabadiliko kwenye Sera ya Faragha ya ASUS
Tunaweza kubadilisha Sera ya Faragha mara kwa mara, tunapendekeza kupitia mara kwa mara Sera ya Faragha iliyowekwa kwenye tovuti zetu. Kwa kupata au kutumia bidhaa na huduma zetu baada ya Sera ya Faragha kusasishwa, ASUS itachukulia kwamba unakubali Sera ya Faragha, ikiwa ni pamoja na masasisho yoyote yaliyomo. Toleo la karibuni zaidi la Sera ya Faragha litapatikana kila mara kwenye ukurasa huu; arafa kama vile kitaarifu cha barua pepe kitatumwa kwako kuhusu mabadiliko yoyote muhimu. Kila mara unaweza kuangalia "wakati ilipoboreshwa" chini ya ukurasa huu kwa ajili ya toleo la karibuni la Sera ya Faragha.
12. Kuwasiliana Nasi
Ikiwa una dukuduku lolote, maswali, maoni au malalamiko kuhusu Sera ya Faragha, au ikiwa unaamini kwamba ASUS haitii Sera ya Faragha, tafadhali kuwa hhuru kuwasiliana na sisi. Ikiwa unafikiri hatuwezi kushughulikia masuala yoyote yanayohusiana na data zako binafsi zilizokusanywa na ASUS, tafadhali tambua kuwa una haki ya kulalamika kwenye mamlaka ya serikali inayoshughulikia ulinzi wa data binafsi katika nchi yako.
ASUSTeK COMPUTER INC. Attn: Personal Data Protection Committee
Anwani: 15, Li-Te Rd., Taipei 112, Taiwan
Barua pepe: privacy@asus.com
Imeboreshwa Mei 23, 2018 na ASUS Personal Data Protection Committee